Simba Sports Club
News

Sakho arejea mzigoni

7 Oct 2021

Kiungo mshambuliaji Pape Sakho, amerejea mazoezini baada ya kupona majeraha na kuwa fiti kwa asilimia 100.

Sakho aliumia enka katika mchezo wa pili wa ligi dhidi ya Dodoma Jiji katika Uwanja wa Jamhuri wiki iliyopita.

Advertisement

Sakho anakuwa mchezaji wa pili kurejea uwanjani baada ya kiungo mkabaji Sadio Kanoute ambaye pia amepona na kurudi uwanjani.

Kikosi chetu kinajiandaa na mchezo wa hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng utakaopigwa nchini Botswana Oktoba 17.

Back to homepage
Share this story