Baada ya kupona majeraha yaliyokuwa yanamsumbua kiungo mshambuliaji Pape Ousmane Sakho sasa anafurahi jinsi ya kiwango chake kinavyozidi kuimarika.
Tangu aliporejea uwanjani mwezi uliopita Sakho amekuwa katika kiwango bora na tayari ameanza kuzikonga nyoyo za mashabiki wetu.
Sakho amesema anajisikia furaha kufanya vizuri na kuisaidia timu kupata ushindi na ndilo jambo lililomleta Simba.
"Unajua nilikaa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na majeraha lakini sasa nimerudi na namshukuru Mungu ninafanya vizuri kuisaidia timu," amesema Sakho.
Katika mchezo wa jana wa nusu fainali ya michuano ya Mapinduzi dhidi ya Namungo, Sakho alichaguliwa mchezaji bora wa mechi baada ya kufunga moja na kusaidia kupatikana kwa jingine lililofungwa na Medie Kagere.