Simba Sports Club
News

Sakho afunguka maana ya ushangiliaji wake

2 Jan 2022

Kiungo mshambuliaji Pape Ousmane Sakho, ameweka wazi maana ya ushangiliaji wake kwa staili ya kukoroga kuwa ni kuongeza kachumbari ndani ya kikosi.

Sakho amefunga bao lake la kwanza la ligi jana dhidi ya Azam FC dakika ya 72 huku akionyesha kiwango safi na kushangilia kwa staili ya kukoroga.

Advertisement

Sakho amesema kama mchezaji kazi yake ni kuongeza kachumbari kwenye kikosi na kuisaidia timu kupata matokeo.

"Ninachomaanisha wakati wa kushangilia baada ya kufunga ni kama vile kuongeza kachumbari ndani ya kikosi ili kuisaidia timu kufanya vizuri. Napenda kuona timu inachangamka inaposhambulia," amesema Sakho.

Back to homepage
Share this story