Simba Sports Club
News

Sakho aanza kuonyesha yake Morocco

14 Aug 2021 By simba 4,195 views

Baada ya kukamilisha usajili kiungo mshambuliaji Pape Ousmane Sakho ameanza mazoezi pamoja na wachezaji wenzake katika kambi inayoendelea nchini Morocco.

Licha ugeni kikosini Sakho ameonyesha kuanza kuzoeana haraka na wenzake kitu mbacho kinaonekana kitakuwa mchango mkubwa kwa timu.

Sakho 24, raia wa Senegal amejiunga moja kwa moja na kikosi kilichopo hapa Morocco akitokea Timu ya Teungueth FC ya nchini kwao.

Advertisement

Sakho ambaye anacheza winga wa kushoto amekuwa mchezaji muhimu wa Teungueth kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho msimu uliopita.

Sakho anakuwa mchezaji wa nne tuliyemsajili msimu huu baada ya Peter Banda, Yusuph Mhilu na Duncan Nyoni.

Back to homepage
Share this story