Simba Sports Club
News

Saba waitwa timu zao za Taifa

9 Nov 2025

Watano wameitwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' ambao ni Yakoub Suleiman, Shomari Kapombe, Wilson Nangu, Morice Abraham na Seleman Mwalimu.

Kikosi cha Taifa Stars kitaingia kambini Novemba 10 kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Kuwait utakaopigwa Novemba 15 nchini Misri.

Advertisement

Mshambuliaji, Steven Mukwala ameitwa kwenye kikosi cha Uganda 'The Cranes' kitakachocheza mechi mbili dhidi ya Chad utakaopigwa Novemba 14 na Morocco, Novemba 18.

Kiungo mkabaji, Naby Camara ameitwa kwenye kikosi cha Guinea ambacho kitacheza mechi mbili dhidi ya Togo, Novemba 15 na Niger, Novemba 18.

Back to homepage
Share this story