Simba Sports Club
News

Rushine De Reuck ni Mnyama

29 Jul 2025

De Reuck (29) raia wa Afrika Kusini ni mlinzi mwenye uzoefu mkubwa wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na hiyo ni moja ya vitu vilivyotushawishi kuisaka saini yake.

Msimu uliopita De Reuck alikuwa anachezea timu ya Maccabi Petah Tikva ya Israel na alikuwa moja ya wachezaji muhimu ndani ya kikosi hicho.

Advertisement

Huu ni usajili wetu wa kwanza kuelekea msimu mpya wa mashindano 2025/2026 na tayari amewasili nchini kuanza maandalizi (Pre Season).

Back to homepage
Share this story