Simba Sports Club
News

Robertinho: Tunahitaji kuyasahau ya Raja tujiandae na Vipers

19 Feb 2023

Robertinho amesema bado tuna mechi nyingine mbeleni kwahiyo ni vizuri kujipanga kuliko kusononeka na matokeo ya jana.

Akizungumzia mchezo wenyewe, Robertinho amesema wachezaji walicheza vizuri lakini walipaswa kufanya zaidi ya walichofanya kwakuwa Raja ni timu kubwa yenye uzoefu.

Advertisement

"Tulicheza vizuri lakini tulipaswa kucheza zaidi ya tulivyocheza kuanzia kuzuia, kukaba mpaka kushambulia hata wachezaji wa pembeni ilitupasa kufanya zaidi. Kipindi cha pili tulitulia tukafanye mambo kwa usahihi lakini bado haikutosha.

"Lakini huu ni mpira na matokeo haya sio ya kushangaza badala yake tunajiandaa na mchezo ujao wa ugenini dhidi ya Vipers wikiendi ijayo," amesema Robertinho.

Back to homepage
Share this story