Simba Sports Club
News

Robertinho: Tuna muendelezo mzuri katika mechi zetu zilizopita

15 Apr 2023

Robertinho amesema katika mechi zetu zilizopita tumekuwa kwenye kiwango bora na tumepata matokeo chanya hivyo imetuongezea morali kuelekea mchezo wa kesho.

Robertinho ameongeza kuwa 'Derby ni Derby' na siku zote inakuwa ngumu lakini anawaamini wachezaji wetu watafuata maelekezo ambayo wamepewa.

"Tuna muendelezo mzuri wa matokeo katika michezo yetu iliyopita, tumepata wiki moja ya maandalizi ya mchezo na wachezaji wote wapo tayari.

Advertisement

"Lengo letu ni kuhakikisha tunashinda kila mechi na kucheza vizuri, nawajua vizuri wapinzani wetu Yanga tunawaheshimu lakini tumejipanga. Mpira kwangu ni sanaa napenda wachezaji wacheze na kuwafurahisha mashabiki pia," amesema Robertinho.

Robertinho pia mewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kuipa sapoti timu kwakuwa wana mchango mkubwa kwa upatikanaji wa ushindi.

"Nawapongeza sana Watanzania kwakuwa wanapenda sana mpira na wanajitokeza wengi sana uwanjani, niwaombe mashabiki wetu waje kutupa nguvu tuwalipe furaha," amesema Robertinho.

Back to homepage
Share this story