Simba Sports Club
News

Robertinho: Tumejipanga kuingia hatua ya makundi kesho

30 Sep 2023

Robertinho amesema timu imepata muda wa kujiandaa na wachezaji wapo kwenye hali nzuri kuhakikisha tunapata matokeo ya ushindi yatakayotuvusha.

Akizungumzia kukosekana kwa mlinzi wa kati, Henock Inonga katika mchezo wa kesho Robertinho amesema "Henock ni beki bora sio Tanzania tu bali Afrika, tutamkosa kesho lakini tayari tumemuandaa mbadala wake na ninaiamini timu yangu."

"Mara zote kocha anahitaji kuwa na wachezaji wake bora lakini katika mpira hili linatokea hata wenzetu Power Dynamos watawakosa wachezaji wao watatu," amesema Robertinho.

Advertisement

Kwa upande wake kiungo mshambuliaji, Clatous Chama amesema kila mchezaji anajua umuhimu wa mchezo wa kesho na yupo tayari kuipigania timu kuhakikisha tunaingia hatua ya makundi.

"Sisi wachezaji tunajua umuhimu wa mchezo wa kesho, tunafahamu furaha ya mashabiki wetu inatutegemea kwahiyo tutajitoa kuhakikisha hilo linatokea ingawa tunajua tutapata upinzani mkubwa," amesema Chama.

Katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Ndola; Zambia kwenye Uwanja wa Levy Mwanawasa tulitoka sare ya mabao 2-2.

Back to homepage
Share this story