Simba Sports Club
News

Robertinho: Timu bora uwanjani imeshinda

10 Aug 2023

Robertinho amesema tulikuwa bora maeneo mengi tukitawala sehemu kubwa ya mchezo huku Singida wakicheza mpira wa kasi na kushambulia kwa kushtukiza.

Robertinho amewasifia wachezaji wetu kwa kazi kubwa waliyofanya huku akimvulia kofia mlinda mlango, Ally Salim kwa kufanikiwa kuokoa penati ya kwanza.

"Lazima nikubali tumepata upinzani mkubwa, Singida wamecheza vizuri lakini sisi tulikuwa bora zaidi yao. Naweza kusema timu bora imeshinda ndani ya uwanja," amesema Robertinho.

Advertisement

Akizungumzia mchezo wa fainali dhidi ya Yanga siku ya Jumapili, Robertinho amesema utakuwa mgumu lakini tupo tayari kuwakabili.

"Itakuwa mechi ngumu, ni Derby na siku zote inakuwa hivyo. Tuna siku siku mbili za kujiandaa kabla ya mchezo," amesema Robertinho.

Back to homepage
Share this story