Simba Sports Club
News

Robertinho awapongeza wachezaji kwa kuipigania timu

24 Oct 2023

Robertinho amesema wachezaji wamepambana na walijitahidi kutafuta ushindi lakini mpira una matokeo ya kikatili wakati mwingine.

Robertinho amewapongeza pia Al Ahly kwa kufanikiwa kutinga nusu fainali ya African Football League (AFL) lakini wamepata upinzani stahiki kutoka kwetu.

Advertisement

"Tulifanya kila tulichopaswa kufanya kutafuta ushindi, wachezaji wamepambana hadi mwisho na tulicheza vizuri pia, haikuwa kazi rahisi, nawaongeza kwa hilo.

"Nawapongeza pia Al Ahly kwa kufanikiwa kutinga nusu fainali, huu ni mpira, tutajipanga wakati mwingine," amesema Robertinho.

Back to homepage
Share this story