Robertinho amesema licha ya ushindi mwembamba wachezaji wamecheza vizuri kwa kufuata maelekezo ingawa tunatumia falsafa mpya.
Robertinho pia amefurahishwa na idadi kubwa ya mashabiki waliojitokeza kuipa sapoti timu huku akiamini baada ya muda mfupi kikosi kitakuwa kimezoeana.
"Nimefurahia ushindi wa leo, na si alama tatu tu zimenifurahisha bali pia jinsi timu ilivyocheza. Tulicheza kitimu, falsafa ni mpya lakini wachezaji wanaielewa.
Advertisement
"Tumewakosa wachezaji watano wa kikosi cha kwanza ambao ni majeruhi wengine wanatumikia adhabu ya kadi tatu za njano lakini bado tumejitahidi kucheza vizuri.
Kuhusu wachezaji wapya tuliowasajili Robertinho amesema; "wamecheza vizuri wamejitahidi kuzoea mazingira haraka hilo pia limenifurahisha."