Simba Sports Club
News

Robertinho afurahishwa na timu licha ya kupoteza dhidi ya Turan

27 Jul 2023

Robertinho amesema tulicheza vizuri kuanzia kwenye kushambulia, kuzuia pamoja na kumiliki mchezo kwa muda mrefu.

Robertinho ameongeza kuwa ubora wa kikosi tulionao sasa anaamini tutafanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na mashindano ya ndani msimu ujao.

"Kwangu siangalii matokeo ya mwisho bali mchezo wenyewe ulivyokuwa. Tumecheza vizuri kuanzia mwanzo hadi mwisho.

Advertisement

"Wachezaji wameonekana wapo timamu kimwili, kimbinu na hilo ni jambo ambalo limenifurahisha. Nawapongeza pia wasaidizi wangu wamefanya kazi kubwa kwa muda mfupi," amesema Robertinho.

Robertinho ameweka wazi kuwa tunahitaji kucheza mechi nyingine moja ya kirafiki mwishoni mwa juma kabla ya timu kurejea jijini Dar es Salaam.

Back to homepage
Share this story