Simba Sports Club
News

Ratiba ya Simba kuelekea Simba Day

31 Jul 2022

Kama ilivyo kawaida yetu wiki moja kabla ya kilele cha Simba Day tunakuwa na matukio mbalimbali ya shuguli za kijamii.

Kesho Agosti Mosi tutakuwa na shughuli ya kusaini mkataba na mdhamini Mkuu M-BET.

Jumanne tutakuwa na zoezi la usafi kwa taasisi mbalimbali nchi nzima.

Jumatano itakuwa zoezi la kuchangia Damu nchi nzima

Ijumaa tunaenda kutembelea Magereza ya Watoto nchi nzima.

Jumamosi - Wachezaji watapewa semina ya mambo mbalimbali ya kijamii.

Jumapili - Dua

Advertisement

Viingilio vya Tamasha letu vitakuwa kama ifuatavyo

Mzunguko Sh. 5000

Viti vya Orange Sh. 10,000

VIP B na C Sh. 20,000

VIP A Sh. 30,000

Platinum Sh. 200,000

Back to homepage
Share this story