Simba Sports Club
News

Ratiba ya Simba kuelekea Simba Day

31 Jul 2022 By simbasc 1,891 views
Leo tumezindua rasmi ratiba yetu yetu ya wiki nzima kuelekea Tamasha la Kimataifa la Simba Day ambalo litafanyika Agoati 8 Uwanja wa Benjamin Mkapa. Kama ilivyo kawaida yetu wiki moja kabla ya kilele cha Simba Day tunakuwa na matukio mbalimbali ya shuguli za kijamii. Kesho Agosti Mosi tutakuwa na shughuli ya kusaini mkataba na mdhamini Mkuu M-BET. Jumanne tutakuwa na zoezi la usafi kwa taasisi mbalimbali nchi nzima. Jumatano itakuwa zoezi la kuchangia Damu nchi nzima Ijumaa tunaenda kutembelea Magereza ya Watoto nchi nzima. Jumamosi  wachezaji watapewa semina ya mambo mbalimbali ya kijamii. Jumapili Dua. Viingilio vya Tamasha letu vitakuwa kama ifuatavyo Mzunguko Sh. 5000 Viti vya Orange Sh. 10,000 VIP B na C Sh. 20,000 VIP A Sh. 30,000 Platinum Sh. 200,000
Advertisement
Back to homepage
Share this story