Power Dynamos imevuka hatua hiyo baada ya matokeo ya jumla ya 2-2 dhidi ya African Stars huku faida ya bao la ugenini ikiwabeba.
Simba ni miongoni mwa timu nane zinazoanzia hatua ya pili kutokana na idadi ya alama nyingi tulizokusanya kwenye viwango vya CAF.
Advertisement
Mchezo wa kwanza utapigwa nchini Zambia kati ya Septemba 15-17 wakati ile ya marudiano itapigwa jijini Dar es Salaam kati ya Septemba 29-30.
Ikumbukwe Power Dynamos tumekutana nao kwenye kilele cha Simba Day, Agosti 6 mwaka huu na kuibuka na ushindi mabao 2-0.