Mkataba huo ni wa miaka miwili hivyo Sandaland atatoa jumla ya Shilingi bilioni nne.
Mtendaji Mkuu wa klabu, Imani Kajula amesema kabla ya kumpa nafasi Sandland Fashion Wear tulifanya utafiti na uzoefu alionao na kipato kikubwa.
Kajula amesema mashabiki wetu wanahitaji jezi zenye ubora na upatikanaji kwa wingi na kufikia Wanasimba wote katika pande zote za nchi kwa haraka kitu ambacho Sandaland wameahidi kulifanyia kazi.
"Ni rasmi Sandaland Fashion Wear ndiye mtengenezaji na msambazaji wa jezi zetu kwa muda wa miaka miwili na kila mwaka atakuwa analipa bilioni mbili.
"Mwaka 2019 tulikuwa tunapata milioni 400, Fred Vunjabei alipokuja akawa anatoa bilioni moja kwa mwaka lakini sasa Sandaland anatoa bilioni mbili kwa mwaka,"amesema Kajula.
Kajula pia amemshukuru Vunjabei kwa uwekezaji wake alioufanya kwa muda wake na amemtakia kila la kheri baada ya kumaliza muda wake.