Dirisha la usajili la CAF limefunguliwa jana Januari Mosi, na leseni ya Mpanzu imetoka leo hivyo atakuwa sehemu ya mchezo wetu wa Kombe la Shirikisho kati ya Simba na CS Sfaxien utakaopigwa Januari 5, nchini Tunisia.
Mpanzu ni miongoni mwa wachezaji 22 waliosafiri kuja Tunisia kwa ajili ya mchezo huo ambao malengo yetu ni kuhakikisha tunapata matokeo chanya.
Advertisement
Katika hatua nyingine kikosi chetu leo jioni kitafanya mazoezi kwanza nchini Tunisia baada ya kuwasili jana.
Taarifa njema ni kuwa mchezo wetu dhidi ya Sfaxien utachezwa katika mji wa Tunis na sio mji wa Sfax ambayo ni makao makuu ya timu hiyo.