Hatua hii imekuja baada ya Maafisa wa CAF kuridhishwa na maboresho yaliyofanywa kwenye uwanja huo kufuatia kufungiwa kipisha marekebisho.
Baada ya taarifa hiyo iliyotolewa na CAF kupitia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Uongozi unawasisitiza mashabiki wetu kutoka sehemu mbalimbali nchini kuendelea kununua tiketi kwa ajili ya mchezo huo.
Advertisement
Viingilio vya mchezo tayari vimetangazwa na tiketi zinaendelea kuuzwa ili kuhakikisha mashabiki wanajitokeza kwa wingi uwanjani kuipa sapoti timu ili kufanikisha malengo ya kutinga nusu fainali.