Simba Sports Club
News

Rasmi Chilunda ni Mnyama

20 Jul 2023

Chilunda ni miongoni mwa washambuliaji wazawa wenye vipaji na uwezo mkubwa na tunaamini atakuwa msaada kwenye kikosi.

Kwa nyakati tofauti Chilunda ameichezea Azam FC tangu akiwa kijana mdogo.

Chilunda ni miongoni mwa wachezaji wazawa waliofanikiwa kucheza soka la kulipwa ambapo amewahi kuzitumikia, CD Tenerife na CD Izarra zote za Hispania pamoja na Moghreb Tetouan ya Morocco.

Advertisement

Baada ya kusajiliwa Chilunda amewaomba Wanasimba tumpokee kwa mikono miwili pamoja na kumuombea ili atimize malengo ya klabu pamoja na yake.

"Sina mengi ya kusema bali Wanasimba wanipokee na waniombee, nimekuja kufanya kazi Simba nitajihid kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu kuweza kushinda kila mechi na mataji klabuni," amesema Chilunda.

Back to homepage
Share this story