Simba Sports Club
News

Rasmi Chama arejea nyumbani

14 Jan 2022

Kiungo mshambuliaji Clatous Chama 'Mwamba wa Lusaka' amerejea tena kikosini kutoka RS Berkane ya Morocco kwa mkataba wa miaka mitatu.

Chama alijiunga na Berkane kutoka kwetu katika usajili wa dirisha kubwa lililopita lakini sasa amerejea tena nyumbani.

Hakuna shaka Chama ni miongoni mwa wachezaji walioweka alama ndani ya kikosi chetu na tuna matumaini naye kutokana na uwezo wake mkubwa dimbani.

Advertisement

Usajili wa Chama ni wa kwanza kwetu katika dirisha hili huku tukitarajia kushusha majembe mengine kabla ya usajili kufungwa.

Malengo ya klabu ni kuhakikisha tunatetea mataji yetu yote tuliyotwaa msimu uliopita, tunaendelea kusuka kikosi ambacho kitatuwezesha kufikia nia yetu. Chama ni mmoja wa wachezaji ambao tunaamini watafanikisha hilo.

Back to homepage
Share this story