Simba Sports Club
News

Rais Samia Mgeni rasmi Simba Day

4 Aug 2023

Simba Day ya mwaka huu ni kubwa na maalum ndio maana tumemuomba Rais Dk. Samia kuwa mgeni rasmi.

Uongozi wa klabu unamshukuru Rais Dk. Samia kukubali mwaliko wetu nakuwa miongoni mwa Watanzania 60,000 watakao hudhuria Simba Day ya mwaka 2023.

Advertisement

Maandalizi ya Tamasha hili la kihistoria yanaendelea vizuri, kila kitu kipo kwenye mstari huku taratibu zikiwa vizuri ikisubiriwa siku yenyewe kufika.

Tayari tiketi za Tamasha zimeuzwa zote hivyo ni wazi mashabiki 60,000 wamethibitishwa kuhudhuria Simba Day 2023 ikiwa ni historia mpya kwakuwa haijawahi kutokea.

Back to homepage
Share this story