Simba Sports Club
News

Rais Samia awapongeza Simba Queens

28 Aug 2022

Queens imeshinda taji hilo jana baada ya kuifunga SHE Corporates kutoka Uganda bao moja katika mchezo wa fainali uliopigwa Uwanja wa Azam Complex.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Rais Samia ametuma salamu za pongezi na kututakia heri katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake itakayofanyika nchini Morocco.

Advertisement

"Nawapongeza wanangu wa Simba Queens kwa ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kwa Wanawake (SAMIA CUP). Mmejenga heshima kwa soka la Tanzania na nchi kwa ujumla.

"Nawatakia kheri katika Ligi ya Mabingwa Afrika (2022 CAF Women's Champions League) itakayofanyika nchini Morocco," ameandika Rais Samia.

Back to homepage
Share this story