Simba Sports Club
News

Rais Samia atupongeza kwa kuifunga Yanga

16 Apr 2023

Katika pongezi hizo alizotuma kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rais Samia amesema mchezo wa Derby unawakutanisha Watanzania wengi kwa wakati mmoja.

"Hongereni Simba kwa ushindi mliopata dhidi ya Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC. Upinzani wenu wa jadi uwanjani ni burudani inayowaleta pamoja mamilioni ya Watanzania kutoka katika kila kona ya nchi yetu, kwa namna ya kipekee," ameandika Rais Samia.

Advertisement

Rais Samia ni mdau mkubwa wa michezo hata katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na Kombe la Shirikisho amekuwa akitoa Sh. 5,000,000 kwa kila bao linalofungwa na wawakilishi wa Tanzania ili kuongeza hamasa.

Back to homepage
Share this story