Simba Sports Club
News

Rais Samia atuma salamu za pongezi za Simba Day

3 Aug 2024

Rais Samia ameongea na Wanasimba moja kwa moja baada ya kumpigia simu Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa Utamaduni na Michezo Gerson Msigwa akiwa ndani ya Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Rais Samia ametupongeza kwa kuendelea kulifanya Tamasha la Simba Day kuwa bora kila mwaka.

Advertisement

"Hongereni sana Wanasimba kwa Tamasha bora la Simba Day. Mwaka jana tulikuwa wote lakini leo imeshindikana kutokana na ratiba kuwa ngumu nimeshindwa kuwa hapo."

"Nafahamu msimu uliopita hamkuwa bora sana lakini yaliyopita si ndwele, nyanyukeni songeni mbele," amesema Dkt. Samia

Back to homepage
Share this story