Simba Sports Club
News

Queens yazidi kujikita kileleni mwa SWPL

14 Feb 2023

Mchezo huo ulianza kwa kasi huku tukimiliki zaidi na kutengeneza nafasi lakini ufanisi wa kuzimalizia haukuwa mzuri.

Kiungo Vivian Corazone alitupatia bao la kwanza kwa shuti kali nje ya 18 dakika ya 42 baada ya kupokea pasi ya kutengewa na Pambani Kuzoya.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi na kuendelea kulishambulia lango la Ceasiaa ambapo dakika ya 67 Asha Mnuka alitupatia bao la pili kabla ya Asha Djafar kutupia la tatu dakika nne baadae.

Advertisement

Asha Djafar alikamilisha karamu ya mabao kwa kufunga bao la nne dakika ya 90 baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Ceasiaa.

Kocha Charles Lukula alifanya mabadiliko ya kuwatoa Pambani, Fatuma Issa, Corazone, Mwanahamisi Omary na kuwaingiza Asha Djafar, Dotto Evarist, Asha Rashid, Joelle Bukuru.

Ushindi huu umetufanya kufikisha alama 22 baada ya kucheza mechi tisa huku tukiendelea kushika usukani.

Back to homepage
Share this story