Simba Sports Club
News

Queens yavunja kambi, wachezaji wapewa mapumziko

31 Aug 2022

Kambi hiyo imevunjwa baada ya kunyakua ubingwa wa Klabu Bingwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kwa kuifunga SHE Corporates kutoka Uganda mwishoni mwa juma lililopita.

Wachezaji watakuwa na mapumziko ya wiki mbili kabla ya kurejea mazoezini Septemba 15 kujiandaa na Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (2022 CAF Women's Champions League) itakayofanyika nchini Morocco kuanzia katikati ya Oktoba hadi Novemba mwaka huu.

Advertisement
Back to homepage
Share this story