Kikosi cha Simba Queens kimetua mkoani Ruvuma tayari kwa kuanza mzunguko wa pili wa Ligi ya Wanawake (Serengeti Lite Women's Premier League) ambapo Jumapili tutaikabili Ruvuma Queens.
Kikosi kimewasili Ruvuma jana ambapo leo kimefanya mazoezi katika Uwanja wa Shule ya De Paul English Medium.
Meneja wa timu Seleman Makanya, amesema kikosi kipo kwenye hali nzuri na morali za wachezaji zipo juu tayari kwa mchezo wa Jumapili.
Advertisement
"Tumefika salama Ruvuma, wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri leo kikosi kimefanya mazoezi kujiweka sawa tayari kwa mchezo wa Jumapili," amesema Makanya.
Queens imeshinda mechi zote 11 za mzunguko wa kwanza na ipo kileleni mwa msimamo ikiwa na alama 33.