Simba Sports Club
News

Queens yatinga Fainali Ngao ya Jamii

9 Oct 2025

Mchezo ulianza kwa kasi tukishambuliana kwa zamu huku safu zote za ulinzi zikiwa makini kuhakikisha wanakuwa salama.

Asha Omary alitupatia bao la kwanza dakika ya 34 baada ya mpira wa adhabu uliopigwa na Jentrix Shikangwa ukapanguliwa na mlinda mlango wa Mashujaa Gelwa Yona kabla ya kumkuta mfungaji.

Aisha Mnunka alitupatia bao la pili dakika ya 85 baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Mashujaa ambao walijichanganya baada ya mpira mrefu kupigwa kutoka katikati ya uwanja na kiungo, Vivian Corazone.

Advertisement

Kocha mkuu, Elieneza Nicolaus alifanya mabadiliko ya kuwatoa Aisha Mnunka na Jentrix Shikangwa na kuwaingiza Janeth Nyagali na Fatuma Issa.

Ushindi huu unaifanya Simba Queens kusubiri mshindi kati ya JKT Queens na Yanga Princess kwa ajili ya mchezo wa fainali.

Back to homepage
Share this story