Simba Sports Club
News

Queens yashusha Straika Mkenya

27 Sep 2022

Jentrix ana uwezo mkubwa kucheza nafasi mbalimbali za ushambuliaji kama namba tisa, winga zote mbili namba saba na 11.

Jentrix amejiunga na Queens akitokea Karakumruk inayoshiriki Ligi Kuu nchini Uturuki ambapo akiwa na timu hiyo amefunga mabao nane na kusaidia kupatikana kwa mengine saba.

Advertisement

Kabla ya kujiunga na Karakumruk, Jentrix alikuwa akichezea Vihiga Queens ya Kenya ambayo msimu uliopita aliiwezesha kuchukua Ubingwa CECAFA huku yeye akiibuka mfungaji bora.

Jentrix anakuja kuungana na Opa Clement, Asha Djafar, Olaiya Barakat, Pambani Kuzoya katika idara yetu ya ushambuliaji.

Back to homepage
Share this story