Queens iko mkoani Iringa kwa kambi ya muda mfupi baada ya kupata mwaliko kutoka kwa Ceasiaa ikiwa ni maandalizi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayofanyika nchini Morocco mwezi huu.
Mshambuliaji Opa Clement alitupatia bao la kwanza dakika ya 19 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na nahodha Fatuma Issa 'Fetty Densa'.
Advertisement
Nyota mpya tuliyemsajili hivi karibuni Jentrix Shikangwa raia wa Kenya alitupatia bao la pili dakika ya 50 na likiwa ni la pili kwake tangu ajiunge na kikosi chetu.
Baada ya mchezo huo kikosi kitaanza safari ya kurejea jijini Dar es Salaam kesho asubuhi na kinatarajia kucheza mechi moja ya kirafiki kabla ya kupaa Morocco.