Simba Sports Club
News

Queens yarejea mazoezini kujiandaa na Determine

31 Oct 2022

Baada ya mchezo wa jana dhidi ya wenyeji ASFAR FC leo wachezaji wameendelea na program ya mazoezi kuweka miili sawa kujiandaa na mchezo huo ambao utapigwa Jumatano saa moja jioni kwa saa za nyumbani.

Wachezaji wote 25 wamefanya mazoezi ya leo na kizuri zaidi hakuna aliyepata majeraha kwenye mchezo wa jana ambayo yatamfanya kukosa mchezo wa Jumatano.

Advertisement

Ingawa tumeshindwa kupata matokeo mazuri kwenye mchezo wa jana morali ya wachezaji ipo juu na wapo tayari kuhakikisha tunapata ushindi ili kufufua matumaini ya kufuzu nusu fainali.

Back to homepage
Share this story