Simba Sports Club
News

Queens yapiga tizi la mwisho Morocco

29 Oct 2022

Wachezaji wote 25 tuliosafiri nao hapa Morocco wamefanya mazoezi na wapo kwenye hali nzuri tayari kwa mchezo wetu wa kwanza wa Kundi A.

Mchezo wetu dhidi wenyeji ASFAR FC utaanza saa nne usiku kwa saa nyumbani Tanzania na maandalizi yake yamekamilika kwa asilimia kubwa.

Advertisement

Morali ya wachezaji ipo juu ingawa ni mara yetu ya kwanza kushiriki michuano hii mikubwa Afrika na matumaini ya kufanya vizuri ni makubwa.

Back to homepage
Share this story