Simba Sports Club
News

Queens yapata ushindi wa jioni mbele ya Mashujaa

18 Jan 2026

Usanase alifunga bao hilo kwa mkwaju wa penati baada ya mshambuliaji Jentrix Shikangwa kufanyiwa madhambi ndani ya 18.

Mchezo huo ulishuhudiwa ukienda mapumziko bila kufungana licha ya kushambuliana kwa zamu na kutengeneza nafasi.

Shikangwa aliipatia Queens bao la kwanza dakika ya 47 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Aisha Mnunka.

Advertisement

Mashujaa walisawazisha bao hilo dakika ya 88 kufuatia kutokuelewana baina ya walinzi wetu.

Ushindi huu unaifanya Simba Queens kufikisha alama 25 ikiwa kileleni mwa msimamo baada ya kucheza mechi tisa.

Back to homepage
Share this story