Michezo ya Ngao ya Jamii ni kiashiria cha kufunguliwa kwa msimu mpya wa Ligi Kuu ya Wanawake 2024/25.
Mchezo huo ambao utakuwa Nusu Fainali ya pili itapigwa Jumanne Septemba, 24 saa 10 jioni katika Uwanja wa KMC Complex.
Advertisement
Mshindi wa mchezo huo atacheza fainali na mshindi kati ya JKT Queens na Ceasia Queens ambao utapigwa Septemba 27 katika Uwanja wa KMC Complex.
Kikosi kinaendelea na mazoezi chini ya Kocha Mussa Hassan Mgosi kikiwa na lengo la kutwaa ubingwa wa taji hili ambalo sisi ndio Mabingwa Watetezi.