Mchezo huo wa watani wa jadi huwa unasubiriwa kwa hamu kubwa na wadau wa soka nchini kwa kuwa unakutanisha timu zenye upinzani na ushindani katika kushindania ubingwa.
Mchezo huo utakuwa ni wa tatu kwa timu zote zikiwa na matokeo ya kufanana hatua inayoongeza hamasa ya mechi yenyewe.
Advertisement
Queens inaendelea na mazoezi katika viwanja vyetu vya Mo Simba Arena chini ya Kocha Mkuu Charles Lukula na wasaidizi wake kujiandaa na mchezo huo muhimu.