Simba Sports Club
News

Queens yamaliza nafasi ya tatu

5 Oct 2024

Kiungo mshambuliaji, Asha Djaffari alitufungia bao la kwanza kwa shuti kali akiunganisha Krosi ya Elizabeth Wambui.

Tulipata bao la pili kupitia kwa, Shajrah Shamte kwa kichwa akiwa katika jitihada ya kuokoa mpira wa kona uliopigwa na Precious Christopher.

Kiungo mshambuliaji, Precious Christopher alitupatia bao la tatu baada ya kupokea pasi nzuri kutoka Kwa Asha Djafari.

Advertisement

Asha Djafar alikamilisha karamu ya mabao kwa kufunga la nne kufuatia mpira uliopigwa vivian corazone kutemwa na mlinda mlango Tausi Swalehe.

Kocha wa Simba Queens alifanya mabadiliko ya kuwatoa Dotto Evarist, Ruth Ingosi na Jentrix Shikangwa na kuwaingiza Wincate Kaari, Fatuma Issa na Asha Rashid

Back to homepage
Share this story