Simba Sports Club
News

Queens yaishushia kipigo kizito Baobab

28 Dec 2023

Joanitah Ainembabazi alitupatia bao la kwanza dakika ya nane baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Dotto Everist.

Bao hilo halikudumu maana dakika ya 15 Elizabeth Edward baada ya kutokea piga nikupige kwenye lango letu.

Asha Djafar alitupatia bao la pili dakika ya 31 baada ya kuuwahi mpira ambao wengi walidhani unatoka na kufunga.

Vivian Corazone alitupatia bao la tatu kutoka katika ya uwanja akipiga shuti kali liliomshinda mlinda mlango wa Baobab Jeanne Pauline.

Advertisement

Baobab walipata bao la pili dakika ya 51 kupitia kwa Daniela Ngoyi aliyejifunga kufuatia kurudisha mpira uliomshinda mlinda mlango, Carolyne Rufa.

Asha Djafar alitupatia bao nne dakika ya 64 kabla ya Asha Rashid 'Mwalala' kukamilisha karamu ya mabao kwa kutupia la tano dakika ya 71.

Queens ilifanya mabadiliko ya kuwatoa Mwanahamisi Omary, Joanitah, Dotto, Djafar na Joelle Bukuru na kuwaingiza Diana Mnally, Elizabeth Wambui, Asha Rashid, Koku Kipanga na Jackline Albert.

Back to homepage
Share this story