Simba Sports Club
News

Queens yaifuata Alliance Mwanza

4 Jun 2024

Queens imeondoka na kikosi kamili na hakuna mchezaji yoyote ambaye atakosekana kutokana nakuwa majeruhi.

Katika mchezo huo tunahitaji alama moja ili kujihakikishia kutwaa ubingwa kwakuwa hakuna atakayeweza kuzifikia.

Kocha Mkuu Mussa Hassan Mgosi amesema mchezo utakuwa mgumu na mara zote Alliance wamekuwa wakitusumbua lakini tumejipanga kuwakabili.

Advertisement

"Tunahitaji kupata ushindi au sare ili kupata nafasi ya kutwaa ubingwa na kurejesha taji letu. Tunaenda kukutana na timu ngumu ya Alliance.

"Tunajua itakuwa mechi ngumu, tunaenda Nyamagana tukiwa na lengo la kutafuta pointi tatu na kurudisha ubingwa," amesema Mgosi.

Back to homepage
Share this story