Simba Sports Club
News

Queens yaichapa Fountain Gate KMC Complex

14 Oct 2024

Elizabeth Wambui alitupatia bao la kwanza mapema kipindi cha kwanza baada ya kupokea pasi ya Asha Djafar.

Kiungo mshambuliaji, Precious Christopher alitupatia bao la pili kwa shuti kali lilomshinda Mlinda Mlango Faraja Ahmady ambalo lilitufanya kwenda mapumziko tukiwa mbele kwa mabao 2-0.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi huku tukitawala sehemu kubwa lakini hata hivyo dakika ya 55 tulifanya kosa ambalo lilisababisha Fountain kupata bao.

Advertisement

Jentrix Shikangwa alikamilisha karamu ya mabao kwa kutupia la tatu dakika ya 83 lililomshinda mlinda wa Fountain Gate.

Kocha Yussif Basigi alifanya mabadiliko ya kuwatoa Wincate Kaari, Ritticia Nabbosa, Asha Mwalala na kuwaingiza Asha Rashid, Jentrix Shikangwa na Mwanahamisi Omary.

Matokeo haya yanatufanya kufikisha pointi sita baada ya kucheza mechi mbili tukifunga mabao sita huku tukiruhusu bao moja

Back to homepage
Share this story