Simba Sports Club
News

Queens yaichapa Bunda Queens

17 May 2025

Mchezo huo ulianza kwa kasi huku timu zote zikishambuliana kwa zamu huku zikipoteza nafasi kadhaa za kufunga ambazo zingewafanya kupata mabao ya mapema.

Bunda Queens walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia wa Monica Samwel kabla Asha Djafar tukipatia bao la kusawazisha muda mfupi baadae.

Aisha Mnunka alitupatia bao la pili lakini halikudumu kwa muda mrefu kabla ya Bunda kusawazisha kupitia kwa Jenipher.

Advertisement

Janeth Nyagali alitupatia bao la tatu na ushindi dakika ya 94 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Jackline Albert.

Kocha wa Queens Yussif Basigi alifanya mabadiliko ya kuwatoa Asha Djafar, Precious Christopher, Jentrix Shikangwa na Elizabeth Wambui na kuwaingiza Janeth Nyagali, Fatuma Issa, Asha Rashid na Jackline Albert.

Matokeo haya yainafanya Queens kurejea kileleni mwa msimamo wa Ligi ikiwa na alama 44 baada ya kucheza mechi 17.

Back to homepage
Share this story