Simba Sports Club
News

Queens yaichakaza Yanga Princess Azam Complex

28 Dec 2025

Mchezo ulianza taratibu huku kila timu ikicheza kwa tahadhari na kushambuliana kwa zamu lakini ufanisi wa kuzitumia nafasi zilizopatikana ukawa mdogo.

Jentrix Shikangwa alitupatia bao la kwanza dakika ya 36 akiwa ndani ya sita baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Elizabeth Wambui.

Dakika ya 63 kocha Mussa Mgosi alifanya mabadiliko ya wachezaji wawili ya kuwatoa Zawadi Usanase na Zainah Nandede na kuwaingiza Elizabeth Joseph na Fatuma Issa.

Advertisement

Aisha Mnunka alitupatia bao la pili dakika ya 69 kwa shuti kali akiwa ndani ya sita baada mpira wa krosi uliopigwa na Elizabeth Wambui kupanguliwa na mlinda mlango wa Yanga kabla ya kumkuta mfungaji.

Zikiwa zimesalia dakika mbili kocha Mgosi alifanya mabadiliko ya kuwaingiza wachezaji wawili Cynthia Musungi na Elizabeth Nashon na kuwatoa Jentrix Shikangwa na Fasila Adhiambo.

Ushindi huu unaifanya Simba Queens kurejea kileleni mwa msimamo baada ya kufikisha alama 15 kufuatia kushinda mechi zote tano za kwanza.

Back to homepage
Share this story