Mchezo huo ni sehemu ya maandalizi kuelekea kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi ya Wanawake Tanzania (TWPL) ambao utaanza kutimua vumbi wiki ijayo.
Katika mchezo huo ambao tulimiliki sehemu kubwa tulikuwa bora karibia kila eneo.
Mabao yetu kwenye mchezo huo yamefungwa na Aisha Mnunka, Jentrix Shikangwa na Zawadi Usanase ambao wote wamefunga mabao mawili kila mmoja huku Elizabeth Nashon akifunga la mwisho.
Advertisement
Hiki hapa kikosi kilichopangwa:
Janeth Shija (Ruth Aturo), Zainah Nandende, Doto Evarist (Zawadi Usanase), Kibo, Ruth Ingosi, Zanga Brice, Vivian Corazone (Nashon), Jentrix Shikangwa, Ochu, Fasila Odhiambo (Elizabeth Wambui), Emeliana Mdimu.