Simba Sports Club
News

Queens yaichakaza Mlandizi Simba Day

3 Aug 2024

Mchezo huo ulikuwa mzuri huku tukitawala sehemu kubwa na kufanya mashambulizi mengi langoni mwa Mlandizi.

Nyota wetu Precious Christopher alifungua akaunti yake ya mabao kwa kufunga bao la kwanza akiwa na kikosi chetu.

Advertisement

Mkongwe Asha Rashid 'Mwalala' aligunga mabao matatu 'hat trick' huku akionyesha kiwango bora.

Katika ushindi huo mnono Shelda Boniface alitupia mabao mawili huku Jentrix Shikangwa akifunga moja.

Back to homepage
Share this story