Mchezo huo ulianza kwa kasi huku timu zote zikishambuliana kwa zamu lakini katika dakika 30 za kwanza hakuna aliyeona lango la mwenzie.
Jentrix Shikangwa alitupatia bao la kwanza dakika ya 36 kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Elizabeth Wambui.
Dakika mbili baadae Jentrix alitupatia bao la pili baada ya kuunganisha mpira wa krosi uliopigwa na Aisha Mnunka.
Zawadi Usanase alikamilisha karamu ya mabao kwa kufunga bao la tatu dakika ya 65 kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Zainah Nandede.
Kocha Mussa Hassan Mgosi alifanya mabadiliko ya kuwatoa Elizabeth Joseph, Elizabeth Wambui, Aisha Mnunka, Fatuma Issa na Vivian Corazone na kuwaingiza Zawadi Usanase, Janeth Nyagali, Cordelia Amarachi na Dotto Evarist.
Ushindi huu unaifanya Simba Queens kuendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa WPL baada ya kufikisha alama 31 kufuatia kucheza mechi 11.