Simba Sports Club
News

Queens yaichakaza Fountain Gate Kwaraa

17 Dec 2025

Asha Ramadhani alitupatia bao la kwanza dakika ya nane baada ya mpira wa adhabu uliopigwa na Jentrix Shikangwa kugonga mwamba wa juu kabla ya kumkuta mfungaji.

Dakika ya 28 Queens ilipata bao la pili baada ya mlinzi wa Fountain Gate kujifunga katika jitihada za kuokoa mpira wa krosi uliopigwa na Shikangwa.

Kocha Mussa Mgosi alifanya mabadiliko ya kuwatoa Elizabeth Wambui na Vivian Corazone na kuwaingiza Zawadi Usanase na Elizabeth Nashon ambao waliongeza kasi ya mashambulizi.

Advertisement

Mshambuliaji Aisha Mnunka alikamilisha karamu ya mabao kwa kufunga bao la tatu dakika ya 80 baada ya shuti lililopigwa na Zawadi Usanase kupanguliwa na mlinda mlango wa Fountain Gate.

Ushindi huo unaifanya Simba Queens kufikisha alama tisa wakiwa wamefunga mabao 10 huku wakiwa hawajaruhusu bao lolote mpaka sasa.

Back to homepage
Share this story