Mchezo huo ulianza kwa kasi huku timu zikishambuliana kwa zamu huku zote zikipoteza nafasi kadhaa za kufunga kipindi cha kwanza.
Kiungo, Vivian Corazone alitupatia bao hilo pekee dakika ya 47 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Elizabeth Wambui.
Baada ya bao hilo tuliendelea kushambuliana kwa zamu lakini timu ilishindwa kutumia nafasi ilizopata.
Advertisement
Ushindi huu umetufanya kufikisha pointi 12 tukiendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa Ligi kufuatia kupata ushindi kwenye mechi zote nne.
Kocha Yussif Basigi alifanya mabadiliko ya kuwatoa Asha Djafar na Jentrix Shikangwa na kuwaingiza Ritticia Nabbosa na Wincate Kaari.