Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo yaliyofanyika katika Uwanja wa Mbweni Veterans na wapo tayari kwa mchezo wa kesho.
Mapema Leo kocha Msaidizi, Mussa Hassan Mgosi aliweka wazi kuwa mchezo utakuwa mgumu kutokana na Yanga kutaka kufuata uteja kwetu lakini tupo tayari.
Advertisement
“Tumefanya maandalizi mazuri, tuko vizuri lakini tutacheza kwa tahadhari kubwa kwa sababu Yanga Princess wamefanya usajili mzuri na wamemrejesha kocha Edna Lema ambaye ni mzoefu wa soka la Wanawake,” amesema Mgosi.
Mchezo huo utaanza saa 10:00 jioni katika Uwanja wa KMC Complex.