Simba Sports Club
News

Queens yafanya mazoezi ya mwisho kujiwinda na Green Buffalos

4 Nov 2022

Uwanja tuliofanyia mazoezi ni maalumu kwa ajili hiyo na upo nje ya dimba ambalo tutalitumia kwa mchezo huo muhimu ambao tunahitaji ushindi ili kufuzu hatua ya nusu fainali.

Wachezaji wote wamefanya mazoezi na wapo kwenye hali nzuri tayari kupambania ushindi na kuzidi kuweka historia kwenye michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

Advertisement

Mchezo wa kesho ni kama fainali na wachezaji wetu wameandaliwa kimwili na kiakili kwa ajili ya kuhakikisha tunashinda ingawa haitakuwa mechi rahisi.

Back to homepage
Share this story