Simba Sports Club
News

Queens yafanya mazoezi ya mwisho kujiandaa na Polisi Bullets

25 Aug 2024

Mchezo huo wa Nusu Fainali ambao tunatarajia utakuwa mgumu utapigwa kesho saa tano asubuhi katika Uwanja wa Abebe Bikila.

Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na hakuna aliyepata maumivu ambayo yatamfanya kuukosa mchezo huo muhimu ambao lengo letu ni kushinda ili kutinga fainali.

Advertisement

Morali za wachezaji zipo juu na kila mmoja yupo tayari kuhakikisha anaipambania timu kufikia malengo yake.

Back to homepage
Share this story